Kocha mpya wa Arsenal amemtaka Mesuit Ozil kuacha kupotea
katika mechi kubwa na hivyo aonyeshe kiwango kinachomfanya alipwe pesa nyingi Zaidi.
Mesuit amekua mchezaji wa kupotea katika mechi kubwa hivyo kuwa
mzigo kwa wachezaji wenzake, “kila mchezaji anahitaji ukomavu na kujituma akiwa
uwanjani na nnje ya uwanja, nahitaji sana hivyo vitu kutoka kwa wachezaji wangu”
Unai.
“ozil ni mchezaji wa kariba ya juu, amekua akicheza namba
kumi mara nyinigine akitokea pembeni hivyo anaweza kuwa chachu ya sisi kwenda
mbele”, aliongeza Unai.
Arsenal inachuana na Chelsea jumamosi majira ya saa moja
jioni huku ikikumbuka kipigo cha mabao mawili bila majibu kutoka kwa Manchester
City, hivyo ushindi wa dhidi ya Chelsea utaleta auheni kwa Mhispaniola huyo na
kwa wachezaji wake pia.
No comments:
Post a Comment