Mmoja wa wamiliki kwa klabu ya Arsenal Stan Kroenke aweka kitita cha paun 556 miilion ili kununua share za mmiliki mwanzake Usmamov na kumfanya awe mmiliki wa klabu hiyo.
Endapo atafanikiwa kufanya hivyo basi Arsenal itakua chini ya mmiliki mmoja kwa maana kwamba maamuzi yote yakua ni ya binafsi bila maoni mengine zaidi ya kampuni ya Kroenke.
Tajiri huyo wa kimarekani ameonesha nia hiyo kwa kusema kua anafanya hivyo kwa sababu anataka kuifanya klabu ya Arsenal kua kubwa na yenye mafanikio kuliko alivo ikuta., na pia inakua ni rahisi kuongoza klabu endapo hakutakua na mtu mwingine anehoji ueledi na maamuzi yako.
Maamuzi hayo yamefanya washabiki wa klabu hiyo kulipuka kwa hasira kwenye mitandao ya jamii kutokana na aina ya umiliki usio kua na tija kubwa kwa klabu ila kwake na kampuni yake.
Ikumbukwe kua mwaka 2017 Kroenke na kampuni yake waliotoa kiasi cha pauni million 3 katika klabu ya Arsenal pasipo maelezo kamili juu ya taarifa ya pesa hizo, hii ilizua mjadala mkubwa juu ya mapenzi yake na klabu hiyo.
Kama akiweza kuinunua klabu ikawa binafsi Kroenke Sports Enterprise (KSE) UK, itaweza kufanya maamuzi yafuatayo
· Malipo ya pesa za kamati na migawanyo mingine bila risiti ya aina yoyote
· Hakutakua na mkutano wa bodi ya wenye hisa na mashabiki
· Kuiweka Arsenal FC kama dhamana ya mikopo atakayo chukua kwa ajili ya bishara zake nyningine.
Pia Stan anasuka mipango ya kununua hisa za Arsenal Supporters Trust (AST) kwa nguvu na hivyo kuwanyima mashabiki nguli wa Arsenal walio na share kidogo ambazo wao wanasema ni kama utamaduni ila sio chanzo cha mapato kutoa mcahngo wao katika klabu.
Maamuzi haya ya Stan yameweshitua wengo hasa mchezaji wa zamani wa Arsenal na England, Ian Wright ambae amendika kwenye ukurasa wake wa twitter akisema “nooooooooooo!” yaan hapanaaaaa!.
Washabiki wengine kama DT wa Arsenal ametoa dukuduku lake kwnye ukurasa wa twitter akisema kua “uki imiliki klabu kwa asilimia 100 si ndio tutakua tumekwisha!! Tunakushukuru David Dein kwa kumtambulisha katika klabu yetu, asante Lady Bracewell kwa kumuuzia share zako na asante pia Wenger kwa kua papet wake na kumfanya atuburuze kwa miaka mingi, sijui tutalitoaje hili jitu ”.
No comments:
Post a Comment