Baada ya mapumziko ya kombe la dunia na uchovu tele wa likizo Gareth Southgate tena atarejea uwanja wa mazoezi wa uingereza, safari hii akiwa na ajenda mpya ya kuipeleka uingereza michuano ya ulaya baada ya kuifikisha England nusu fainali ya kombe la dunia anakutana na kiungo wa ajabu ”Xavi mpya”.
Umaridadi wa pasi, uwezo wa kuchekesha timu na ushupavu mkubwa ndio uliofanya timu pinzani ya Chelsea kupata tabu kwel. Akichukua nafasi ya David Silva, Foden ameonyesha kiwango bora kabisa dhidi ya viungo wazoefu wa Chelsea na kuwafanya waonekane wachovu dhidi yake.
Kinda huyu mwenye miaka kumi na 18 alichekecha ngome ya Chelsea na kufanikisha upatikanaji wa goli ya kwanza kwa timu yake, Foden ana kila kitu ambacho Southgate na Pep hua wanakitaka kwa mchezaji na hivyo kumfanya kocha huyo wa England kua na shauku ya kombe la mabingwa ulya.
Baada ya mda mrefu uingereza hawakua na kiungo mwenye uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira, isitoshe uwezo pia wa kurejesha mpira kutoka timu pinzani, hivyo kumfanya awe Xavi wa uingereza, nafikiri tusijipe moyo sana yaweza yakawa yale yale ya Jack Wilshere au Jack Greylish lakin tuombe yasijrudie na msimu ndo huoooo una anza…
No comments:
Post a Comment