Ajenti wa kiungo wa Manchester United ameshusha bomu baada kusema kuwa anahitajia mteja wake aruhusiwe kihama Manchester United na kujiunga na klabu ya Barcelona.
Mino Raiola ambaye ni mmiliki wa wachezaji wakubwa duniani ameonyesha kusuka mbinu za kumng’oa kuingo huyo kutoka Manchester United na Kumkabidhi kwa miamba ya Hispania, Barcelona.
Ikumbukwe kuwa Paul pogba alijiunga na Manchester United akitoke Juventus kwa kitita cha puni 89 million misimu miwili ilio pita lakin hakujaweza kuonyesha kiwango ambacho kilii fanya Machester United kumrejesha.
Ingawa Manchester imesisitiza kuwa Paul hauzwi kwa kiasi chochote klabu ya Barcelona imetoa kiasi cha pauni 44 milion pamoja na wachezaji wawili ofa ambayo inaweza kuwavutia mashetani hao.
Hata hivyo uhusiano wa kocha wa Manchester United dhidi ya Pogba umezidi kuzorota baada ya siku za karibuni kushusha kijembe akisema ” Sio kazi yetu kumfanya Pogba awe bora ila ni kazi yake kujifanya kuwa bora”, nah ii ilikua baada ya maaniki ya Pogba na timu yake ya taifa.
Wakati huo kiungo mwenzake wa Manchester United nemanja Matic atakosekana mwanzoni mwa msimu kutokana na majeruhi ya mgongo hivyo kumfanya abakiwe na viungo wachache wa kati.
Rojo nae ahusishwa kuihama Manchester United na kuelekea Goodson park kunako Everton la sivyo Everton wataelekeza nguvu zao kumnasa Yerri Mina.
No comments:
Post a Comment