Siri ya mafanikio Manchester City 2017/2018 - spn5swahili

Breaking News

test banner

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, August 17, 2018

Siri ya mafanikio Manchester City 2017/2018


Ni kama uwanja wa dansi, Pep anenda anenda mbele hatua tano na kisha kurud hatua nne, ankaa kisha ananyanyuka huku akitafuta maneno ya kujazia kingereza chake hafifu anafoka tena, Sane akiwa kimya kasimama, De-Bruyne yuko kimya mikono machoni, Silva kaegemea ukuta huku kaangalia chini.


Wachezaji na timu nzima ya ufundi ya Manchester City wakionekana kuzoea hali hii kwani si mara ya kwanza kutokea, ilitokea wakati wa mapumziko za kipindi cha kwanza cha fainali ya kombe la karabao dhibi ya Arsenal huku Manchester city wakiwa wanongoza goli moja bila.

Pep anataka umakini, anataka ufanisi na yote anataka ushindi kwa kila mechi hayo ni baadhi ya machache unayo weza kueleza juu ya mhispaniola huyu.

Katika mapunziko ya mechi yao dhidi ya Manchester United ambapo kila mchezaji alidhani mechi hiyo wameshinda na kunyakua kombe baada ya wao kuwa mbele kwa mabao mwaili bila ilizua mjadala mkubwa baada ya mechi kuisha, kwani Manchester United walirejesha mabao yote mawali na kuongeza la tatu la ushindi.


Hali katitka vyumba vya kubadilishia vya Man City ilikua tete huku Company na Delph wakionekana wenye sauti kubwa Yaya toure akiwa na mchango pia katika vyumba hivyo.’si ni wa hovyo!....kipa wa hovyo, mabeki wa hovyo,viungo wa kati wa hovyo na washabuliaji wa hovyo pia.’ Alisikika delph.


Wakati huo nahodha wa timu hiyo akijaribu kuwatuliza kwa maneno ya busara “jamani sisi ni wachezaji wazuri, tangia msimu umeanza tumecheza vizuri hadi hapa tulipo ila leo tumefungwa na sio kitu kizuri labda inawezekana kwasababu ya uchovu” alinena nahodha huyo.
“Tumechoka? Hapana sisi ni wapuuzi…kipindi cha pili tuliacha kukimbia, tuliacha kucheza hii haikubaliki” aling’aka Delph.

Baada ya kuzozana wao kwa wao Pep aliingilia kati na kusema ”mpira sio maua, mpira sio kwenda likizo ila mpira ni mchezo wenye changamoto nyingi cha msingi ni wachezaji kujitambua kama wa kimataifa na kusimamam kidete kutoruhusu hali hii kutokea tena”.


Umoja, mshikamano na hari ya ushindi ndio vitu ambavyo Pep anaweka kwa wachezaji wake na hivyo kuwafanya wajiskie vibaya sana washipo shinda na pia kuongeza juhudi pia wanaposhinda ili washinde Zaidi.
Itaendelea……….

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages