Kocha wa Arsenal amesema maamuzi ya kuendelea na kipa Peter Cech
mi mwepesi na haitaji kuumiza kichwa, ‘ni rahisi tu nitabaki na Peter kama goli
kipa wangu namba moja’, alisema Unai. Kwa maana nyingine kipa mpya wa klabu
hiyo Leno atarndelea kusugua benchi kama kawaida.
Maneno hayo yamekuja baada ya kipa kuyo kuvurunda mechi ya
kwanza ya msinu dhidi ya
Manchester City, kipa huyo alifanya makosa ambayo
yange igharimu timu na hivyo kuibua maswali mengi juu ya uwezo wake.
Kocha Unai aliejiunga na klabu hiyo majira ya joto alikuja
na mfumo mpya amabao inahitaji wachezaji kuanzisha mashambulizi kwankuanzia
nyuma huku mfumo huo ukiwa na changamoto kubwa kwa wachezaji hasa mabeki na
kipa.
Peter Cech alijiunga na Arsenal akitokea Chelsea ambako aliitumikia
klabu hiyonkwa miaka kumi ma moja na kufanikiwa kiutwaa mataji manne ya ligi kuu na moja la
ligi ya mabingwa ulaya.
Arsenal wanakutana na Chelsea kesho katika uwanja wa
Stanford Bridge huku Arsenal wakiwa na historia mbaya uwanjani hapo wakiambulia
ushindi mmoja tu ndani ya miaka takriban mitano ushindi wao wa mwisho ulikuja
mwaka 2010 walipo ifunga chelsea bao tano tatu.
No comments:
Post a Comment