Mastaa walio katika mtihani wa kuonyesha cheche zao baada ya kua na msimu mbovu wa mwaka 2017/2018…je Pogba ataonyesha keke zake za kombe la duinia?
Msimu ujao uko njian na presha inawakabili baadhi ya mastaa wakiwemo
· Wilshere ambaye alikabiliwa na majeruhi misimu mitatu yalioisha? Ataweza kurejesha form yake na club ya West Ham
· Je Paul ataonyesha cheche za kombe la dunia?
· Mesuit Ozil ata hamishia nguvu zake kweny ngazi ya club baada ya kuachana na timu ya taifa?
· Na wnengine kama Morgan Schneiderlin, Jonny Evans na Toby Alderweireld.
JACK WILSHERE(WEST HAM).
Msimu wa mwaka 2011 kiungo wa Barcelona alikili kua jack wilshere ni mchezaji mwenye kiwango cha juu sana baada ya kiungo huyo kupata upinzani mkali pindi timu hizo zilipo kutana katika ligi ya mabingwa.
Wilshere aligubigikwa na majeruhi makubwa misimu ilifuta na kufanya
Kiwango chake kuporomoka kwa kiasi kikibwa, kiungo huyo wa zamani wa arsenal amehama klabu yake ya Arsenal na kujiunga na wagonga nyundo wa London(West Ham) na ana deni kubwa la kuonyesha cheche zake na club yake hiyo mpya..
PAUL POGBA(MANCHESTER UNITED)
Linapokuja suala la kiwango kushuka na kupanda, Paul hatakua na upinzani kutoka kwa wachezaji wengine.
Mcehzaji huyu wa Manchester alikua na msimu mbovu kabisa na ikapelekea kutofautiana na manager wake na kupelekea kukaa benchi mechi kadhaa, lakini katika fainali ya kombe la dunia aliibuka kua mchezaji mwenye kiwango maridadi kabisa na kupelekea wakashinda kombe hilo.
Hivyo anawajibu mkubwa wa kuakisi kiwango cha kombe la dunia kama anahitaji kuandelea kuvaa jezi ya Manchester…
MESUIT OZIL (ARSENAL)
Mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu sana, Mjerumani huyu alisajilwa na Arsenal mwaka 2014 kwa ada ya paund 42 milion akitokea Madrid. Tangu kutokea Madrid Mesuit hajaonyesha kiwango kilochoifanya Madrid kutwaa ligi ya mabingwa.
Hivyo msimu huu Mesuit ana kibarua kigumu chini ya kocha mpya wa arsenal Unai. Je atafaniskisha kurejesha kiwango chake baada ya kuchana na timu ya taifa ya Ujerumani? Au ndo tutegemee Ozil yule mvivu uwanjani.
DANIEL STURIDGE(LIVERPOOL).
Mchezaji huyu wa zamani wa Chelsea kapewa nafasi mpya na kocha wa Liverpool Jurgen klop baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiwa na liverpool katika maandalizi ya msimu ujao (pre-season), Sturridge kaandamwa na majeruhi tangu kujiunga na clabu ya liverpool na kumfanya apoteze nafasi yake mbele ya mbrazil Firmino.
Msimu huu utakua na umuhimu mkubwa sana kwa sturridge kufufua ndoto zake za kucheza kombe la dunia kwa mara ya mwisho katika maisha yake ya soka.
BENJAMIN MENDY (MANCHESTER CITY).
Alikuja na moto baada ya kutokea Monaco na kumfanya kua kipenzi kikubwa cha mashabiki wa Man city, lakini alipata majeruhi makubwa ya goti na kumfanya akose msimu mzima.
Anaonekana atarejea nafasi yake ya mlinzi wa pemebeni wa ndani ya kikosi cha pep na anatumainiwa kurejesha makali yake yaliomfanya anunuliwe kwa ada ya paund million 56.
No comments:
Post a Comment