Baada ya kuona ndoto zake za kurudi nyumbani kukipigia Real Madrid kufifia kipa huyo wa matajiri wa London hakufika uwanja wa mazoezi wa Chelsea na hivyo kuibua maswali mengi kwa washabiki.
Chelsea imejaribu kumshawishi Thibaut kuendelea kubakia na miamba hao wa uingereza kwa kumuongezea mshahara na kufikia paun 200,000 kwa wiki lakini juhudi zao zimegonga mwamba.
Thibaut anataka kulazimisha uhamisho wake kutoka katika klabu hiyo ili ajiunge na klabu ya Real Madrid, huku Chelsea wakiwa tayari kunruhsu tu endapo wata pokea dau la paun 45 millioni.
Wakati huo huo Chelsea yamnyemelea kipa wa Leicester, Schmeichel na jack Butland kama mbadala wa Courtois kama endapo ataondoka.
No comments:
Post a Comment