Majogoo wa Anfield wakamilisha maandalizi ya msimu wa 2018/2019 kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Torino huku wachezaji wageni wote wakianza katika mechi iyo.
Magoli yakifungwa na Roberto Firmino, Gini Wijnaldum na Daniel Sturridge wakifuta makosa Farbhino alie kosa penati huku goli la machozi la torino likifungwa na Andrea Belotti.
Golikipa Alisson, na mbrazili mwenzie Brazilian Fabinho, Swiss winger Xherdan Shaqiri na kiungo matata mbwa wa vita Naby Keita (wakiwa na thamani ya paundi 170 million kwa ujumla) walianza mechi hiyo wakipokelewa kwa shangwe za hali ya juu na mashabiki wa majogoo hao.
Liverpool wataanza ligi kwa kukabiliana na wagonga nyundo wa London West Ham siku ya jumapili 12.
Kipa mpya Alison atachukua nafasi ya Karius ambaye makosa yake yaliikosesha timu hiyo kunyakua ubingwa wa ulaya mbele ya Real Madrid, huku kiuongo mahiri Naby Keita takua akirandan randa dimbani akichukua nafasi ya Emre Can alie timkia Juventus.
Kocha wa Liverpool Jurgen klop kafanya usajili wa nguvu na kuifanya timu hiyo kua na tishio katika safu zote na hivyo wachambuzi wengi kuipa nafasi ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu England na matumaini ya kufika fainali ya ubingwa wa ulaya kwa mara ya pili.
“sikushangaa, sikua na hofu na nlitegemea ushindi huu, hii itawasaidia wachezaji kuwa na ari ya kujiamini na muamko wa ushindi”, alisema Klop.
No comments:
Post a Comment