Mabingwa hao wa ulaya wali hitimisha ziara yao katika bara ya marekani kwa kuinyuka Roma klabu ya Italia kwa mabao mawili kwa moja katika uwanja wa New Jersey, mabao yakifungwa na Garath Bale na Asensio huku kakufutia machozi la Roma likifungwa na Kelvin Stootman .
Julen Lopetegui alitupa uwanjani kikosi kizito kilicho husisha Navas,Carjaval (Sergio Lopez 71), Nacho (Raul De Tomas 81), Ramos (Marcos Llorente H-T), Reguilon (Odegaard 71); Ceballos (Jose Leon 71), Kroos (Sanchez H-T), Isco (Valverde 56); Bale (Vazquez 56), Benzema (Vinicius 57), Asensio (Borja Mayoral 57).
Mabingwa hao walioneka katika kiwango maridhawa kabisa huku wakicheza mpira wa pasi fupi fupi na kasi ya aina yake hivyo kuwapa wakato mgumu wapinzani wao.
No comments:
Post a Comment