Mshambuliaji Lucas Perez ajiunga rasmi na klabu ya wagonga nyundo wa London,West Ham kwa kitita cha paundi million 10 akitokea Arsenal, Perez alijiunga na Arsenal msimu ulio isha kwa mkataba wa miaka mitatu ambapo msimu mmoja alirudishwa kwa mkopo katika klabu yake ya zamani ya Derpotivo.
“Nina furaha sana kujiunga na klabu hii, West Ham ni klabu kubwa sana na ina mashabiki wazuri na pia ina uwanja mzuri”, aliongeza mchezaji huyo raia wa Hispania.
Kukamilika kwa dili hilo kumeifanya West Ham kufikia idadi ya wachezaji nane akiwemo Jack Wilshere ambaye alikua na mchango mkubwa kumshawishi Lucas kujiunga na klabu hiyo. Wachezaji wengine walio jiunga na West Ham ni Ryan Fredericks, Lukasz Fabianski, Issa Diop, Wilshere, Andriy Yarmolenko, Fabian Balbuena na Felipe Anderson.
No comments:
Post a Comment