Santi Carzola ni jina ambalo si geni miongoni mwa wapenzi wa mpira wa miguu duniani, mhispaniola huyu kajizolea umaharufu mkubwa kutokana na uwezo wake uwanjani huku sifa kubwa ikiwa ni kutumia miguu yote kwaustadi wa hali ya juu asakatapo kabumbu.
Carzola karejea katika klabu yake ya zamani Villareal akitokea Arsenal akiw amchezaji huru baada ya kuitumikia klabu hiyo ya washika bunduki wa London takirbani misimu sita huku msimu wake wa mwisho ukiandamwa na majeruhi makubwa yalio muweka nnje siku zipatazo 646.
Kuingo huyo mwenye miaka 33 alitambulishwa jana katika klabu yake kwa staili ya aina yake mbele ya mashabiki takribani 4,500 wa klabu hiyo, Santi alionekena ndani ya umbo lenye mithiri ya tanki likiwa na moshi mweupe huku akiwa amekunja mikono na tabasamu maridhawa kabisa.
Mwaka mmoja ndio mkataba utakao muweka Carzola klabuni hapo.”Nmerudi nyumbani nawashukuru uongozi wa Villareal kwa kunipokea kwa mikono miwili” alisemaSanti.
No comments:
Post a Comment