Mchezaji wa zamani wa Arsenal na England ameponda kocha mpya
wa Arsenal, Unai baada ya kichapo kutoka kwa mabingwa wa ligi hiyo Manchester City.
Tony amenshangaa kocha huyo kwa kuwa na mtindo wa kubadilisha badilisha
wachezaji wakati wa “pre season”, na kusema kuwa haikuwa na umuhimu wa kufanya
ivyo bali angechagua kikosi ambacho angeweza kuanza nacho katika msimu mpya.
Pia ameongeza kuwa ni jambo zuri kuadilisha mfumo lakini
itachukua muda wachezaji kuzoea mfumo mpya nah ii ni kutokana na makosa
yalionekana wakati wa mechi,”mfumo mpya ni changamoto ukizigatia wacheza
walikua wamezoea mfumo wa Arsene Wenger” aliongeza Adams.
Tony Adams ameichezea Arsenal katika miaka ta tisini pamoja
na mwanzoni mwa miaka ya 2000 huku akujizolea umaarufu mkubwa akiwa na washika
bunduki hao wa London akishinda vikombe vya ligi kuu vinne.
Arsenal itakabiliana na Chelsea katika uwanja wa Stanfrod Bridge
jumamosi hii huku kocha huyo akiwa na matumaini Arsenal haita kuwa dhaifu kama
mechi ya Manchester City.
No comments:
Post a Comment