Nedved mchezaji wa zamani wa Juventus na mkurugenzi amesema
kuwa wanayo furaha sana kumsajili mchezaji bora wa dunia Christiano Ronaldo, na
kuwa yeye atakua chachu ya kufanikiwa katika mbio zao za kuinyakua ligi ya
mabingwa msimu huu.
Ronaldo mwenye miaka 33 alisajiliwa na Juventus akitokea
Real Madrid kwa kitita cha paundi million 108 na alionyesha cheche zake hapo
jana alipofunga bao katika mechi ya dhidi ya juventus ndogo.
‘dunia inatambua uwepo wetu katika ushindani wa soka ulaya’
aliongeza Nedved. Juventus itafungua ligi katika mechi dhidi ya Chievo, mechi
ambayo Christiano ataanza na itakua mechi yake ya kwanza ya ushindani.
No comments:
Post a Comment